Katika jamii yeyote wa wanadamu ambao wana ishi pamoja na kushirikiana,marafiki ni watu ambao wana kuwepo.Hawa wanakuwa watu wa karibu na mtu fulani kwa shida na raha.Tunategemea kuona marafiki wakiwa wana furaha na amani pia waki shirikiana katika masuala mbalimbali katika maisha.
Yapo baadhi ya maswali ya kujiuliza mtu mwenyewe katika nafsi yako.Maswali hayo ni;Je urafiki nilionao na mtu fulani una faida au hasara? Lakini pia vema kujiuliza kama Urafiki huo katika maisha yako hauwezi kuwa na madhara.Madhara hayo yanaweza kuwa chanya au hasi.Hii ina maana kuwa ni vizuri kutambua umuhimu wa urafiki huo na athari zake.
Kwa sasa ulimwengu umekuwa katika matatizo mengi yanayotokana na urafiki.Matatizo haya yanaweza kuepukwa kwa wanadamu kuwa waangalifu na watu ambao wana kuwa katika mahusiano ya urafiki.Uwe urafiki wa kawaida au wa kimapenzi.Hii itasaidia sana kujenga jamii ya marafiki walio bora na kuwa na urafiki mzuri na wenye mafanikio kwa pande zote husika.
No comments:
Post a Comment