Monday, June 27, 2011
‘Shaggy’ alivyojiachia ndani ya Visiwa vya Zanzibar
Pichani ni mwanamuziki wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard ‘Shaggy’ alivyojiachia ndani ya Visiwa vya Zanzibar wakati alipokuwa akielekea wa ajili ya tamasha la filamu za nchi za majahazi maalufu kama (Zanzibar International Film Festival-ZIFF) lililofanyika ndani ya Ngome kongwe na kufurika mamia wa mashabiki kumshuhudia mjamaika huyo anayeishi marekani.
SHAGGY ATAWAZWA KUWA CHIFU NA BALOZI WA KABILA LA WASUKUMA BUJORA, MWANZA
SHAGGY AKIWASILI MJINI MWANZA
Mwanamuziki Shaggy wa Marekani akiondoka kwa kucheza huku akiwa ameshikilia usinga na kusindikizwa na vigoli wa kabila la kisukuma wakati alipokuwa akiondoka katika eneo la tukio mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma, katika tamasha la ngoma za asili la Siku ya Mavuno yaani (Bulabo) kwa Kisukuma lililofanyika katika kijiji cha Kisesa mahali ambapo pana makumbusho ya Bujora yaliyohifadhi tamaduni zote za kabila la wasukuma.
Mwanamuziki Shaggy akishangilia mara baada ya kumtawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika kijiji cha Kisesa.
Mwanamuziki Shaggy akishangilia mara baada ya kumtawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika kijiji cha Kisesa.
HAYA NDO MAMBO YA USIKU WA KHANGA ZA KALE
Pichani ni wanamuziki wa wana Njenje Band-The kilimanjaro wakiwa wametinga Khanga za kale wakati wakifanya onesho pale Salender Bridge Club
Washiriki wengine wakifurahia usiku wa kale.
Dida nae hakuachwa nyuma kwenye usiku wa khanga za kale
Thursday, June 23, 2011
AFRICA MAGIC SWAHILI KUANZA KUONEKANA LIVE JULAI MOSI MWAKA HUU…!!!
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA Yustus Mkinga akifafanua juu ya hakimiliki za kazi za wasanii nchini katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI zilizofanyika jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Baadhi ya wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakishuhudia uzinduzi huo. |
![]() |
| Mmoja wa watengezaji filamu za kibongo maarufu kwa jina Mtitu akitoa hoja katika uzinduzi wa kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI zilizofanyika jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Baadhi ya wasanii wa filamu za kibongo waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo. |
![]() |
| Muigizaji na Mtengenezaji Filamu za kibongo Steven Kanumba hakuwa nyuma katika kuchangia hoja mbalimbali kwenye uzinduzi huo. |
Wednesday, June 22, 2011
Zawadi Za Vodacom Miss Mwanza zatangazwa
Hatimaye Zawadi za washindi wa Vodacom Miss Mwanza 2011, zimetangazwa leo katika ukumbi wa Hoteli mpya ya Gold Crest iliyopo katikati ya jiji la Mwanza. Akitangaza zawadi hizo Katibu wa Sisi Entertainment Mukhsin Mambo maarufu Mc Stopper ameeleza, kifuta jasho kwa washiriki nafasi ya sita hadi ya kumi na nne watapata Tsh. 100,000/=
Nafasi ya Tano- 200,000/= Nafasi ya Nne- 200,000/= nafasi ya Tatu- 300,000/= Nafasi ya Pili- 500,000/= na Vodacom Miss Mwanza 2011- 1,000,000/=
Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Miss Mwanza kuzawadiwa donge nono la Tshs. 1,000,000/=
Askofu Wa TAG Aiponda Bajeti Ya Serikali, Asema Haina Lengo La Kumkomboa Masikini
| HUKU wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hasa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wakiipinga mapendekezo ya bajeti ya serikali kwwa mwaka wa fedha 2011/2012 iliyowasilishwa bungeni na waziri wa fedha na uchumi Mustafa Mkulo ,askafu wa kanisa la Tanzania Assembulise Of God (TAG) jimbo la Iringa Jonas Mkane (pichani) ameipinga bajeti hiyo kuwa haijalenga kumkomboa mwananchi wa kawaida. Pamoja na kuipinga bajeti hiyo pia askofu huyo aliitaka serikali kuwashughulikia vikali mafisadi ambao ndio wanafanya watanzania kuishi maisha magumu. Katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kufungua semina ya wachungaji wa jimbo la Iringa iliyofanyika TAG Mlandege ,askofu Mkane alisema kwa upande wake anaona kuwa bajeti hiyo haijalenga kumkomboa mwananchi wa kawaida . Alisema kwa upande wake alifikiri kuwa kabla ya kutenga bajeti hiyo serikali inapaswa kushughulika na watu wachache ambao wamekuwa wakiichakaza nchi kwa kuendekeza ufisadi na baada ya hapo kukaa chini na kutenga bajeti ya wananchi itakayowatoa katika dimbwi laumaskini ila kuendelea kutenga bajeti hiyo na kuwakabidhi mafisadi ni kumkomoa mwananchi. "Mimi nadhani kabla ya kutenga bajeti hiyo serikali inageanza kushughulika na watu wachache ambao wanafanya ufisadi ndani ya Taifa ambao wanafahamika soma zaidi |
Subscribe to:
Posts (Atom)



















