Thursday, June 23, 2011

AFRICA MAGIC SWAHILI KUANZA KUONEKANA LIVE JULAI MOSI MWAKA HUU…!!!

Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA Yustus Mkinga akifafanua juu ya hakimiliki za kazi za wasanii nchini katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Katikati ni Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Peter Fauel akifuatilia kwa makini uzinduzi wa AFRICAN MAGI SWAHILI uliyofanyika katika Hoteli ya MovenPick jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kitaanza kuonyeshwa rasmi Julai 1 siku ya Ijumaa kuanzia saa 11 jioni kupitia Channel 127.

Mkurugenzi wa MNET Africa Biola Alabi akifungua rasmi Channel  ya filamu za Kiswahili itakayojulikana kama AFRICAN MAGIC SWAHILI itakayokuwa ikipatikana katika Channel 127 kuanzia saa 11 jioni mpaka saa 5 usiku katika sherehe za ufunguzi zilizofanyika kwenye Hoteli ya  MovenPick jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi.

Baadhi ya wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakishuhudia uzinduzi huo.

Mmoja wa watengezaji filamu za kibongo maarufu kwa jina Mtitu akitoa hoja katika uzinduzi wa kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Msanii Mkongwe wa filamu nchini Natasha maarufu kama Mama Monalisa akiwashukuru MNET AFRICA kwa kutambua na kuendeleza kazi zao nchini na Afrika Mashariki katika uzinduzi wa Kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wasanii wa filamu za kibongo waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo cha AFRICA MAGIC SWAHILI iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo.

Muigizaji na Mtengenezaji Filamu za kibongo Steven Kanumba hakuwa nyuma katika kuchangia hoja mbalimbali kwenye uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment