Tuesday, June 14, 2011

TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA TAREHE 16-04-2011

TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA TAREHE 16-04-2011

Kikao kilifanyika NEW MSASANI CLUB kuanzia saa 7.00 mchana mpaka saa 10.20 jioni.Kilimujuisha wana klabu wa Mkoa wa Dsm wanawake kwa wanaume ambao walijadili masuala mbalimbali ya klabu,kuanzia mwanzo wake,ilipo sasa na mwelekeo wa badae na kufikia maazimio yafutayo;
  • VI0NGOZI WA KLABU-Kwa sasa hakuna sababu ya kuchagua viongozi ila wawepo viongozi wa muda ambao wata hakikisha kuwa shughuli za kila siku za kundi zinaendelea.Viongozi kamili wa kundi wachaguliwe badae.Hivyo waliwateua NELSON JOHNSON,BAB CHICHARITO NA JOYCE MAHILA kuongoza klabu kwa sasa.
  • JINA LA KUNDI-Imeafikiwa kuwa wana kundi wapendekeze jina jipya la kundi hili.Kwa sasa jina la kundi hili linajenga picha ya kundi la kimapenzi jambo ambalo sio sahihi.Wana kundi wapendekeze jina jipya wakizingatia kuwa kundi litajihusisha hata kujadili masuala yote ya kisiasa, kijamii,kielimu,kiuchumi,kimahusiano,kiafya na kibiashara.Huku wakizingatia taratibu,kanuni zetu za kuwa wastaharabu katika kutoa mawazo.
  • KUONGEZA IDADI YA WANA KIKUNDI-kikao kilipitisha kuongeza idadi ya wanachama hata kama wako mikoani(nje ya DSM).Wanachama wataopewa nafasi kuingia katika kundi letu wanapaswa kuzingatia taratibu zetu na wale watakao waongeza wawape japo malezo mafupi juu ya kundi hili.
  • MADA ZINAZOWEKWA KATIKA KUNDI(STATUS)-zizingatie na kuheshimu watu wote.Humu ndani wapo watu wa jinsi tofauti,imani tofauti,mahusiano tofauti na hata historia ya nyuma isiyofanana.UVUMILIVU,KUREKEBISHANA,KUONYANA NA KUSAMEHE ni mambo ya msingi pale mnapotofautiana kimawazo.MATUSI,KASHFA,DHARAU NA KUCHAFUANA SIO MAHALI PAKE.Ni vema tukaheshimina na kujitahidi kuchangia katika mada mbalimbali.
  • NIDHAMU-Uongozi hautasita kumfuta mwana kikundi pale ambapo atapewa onyo na ushauri na kuonekana anaendelea kuwa tatizo katika kundi.Hii sio sehemu ya kutafuta umaarufu bali kujenga jumuiya bora na imara kwa maendeleo yetu vijana.
Uongozi unawashukuru wana klabu wote ambao walijitokeza jana katika kikao licha ya kuacha shughulli zao mbalimbali.Hii inaonyesha umoja na mshikamano kati yetu anbao utafanya kundi letu liendelee mbele.
Uongozi utapokea mawazo na ushauri wenu wakati wowote bila kujali chochote maana sisi wote ni kitu kimoja.KARIBU KIKAO KINACHOFUATA TAREHE 7/05/2011 SAA 9.00 ALASIRI,NEW MSASANI CLUB
Naomba kuwasilisha
UONGOZI

No comments:

Post a Comment