Tuesday, June 14, 2011

TAARIFA YA UONGOZI WA MUDA NA HALI YA KIKUNDI KWA SASA

TAARIFA YA UONGOZI WA MUDA NA HALI YA KIKUNDI KWA SASA


Kwa muda wa miezi 3 sasa group limekuwa likiongozwa na viongozi wa muda ambao walichaguliwa wakati wa kikao cha kwanza cha wana klabu wa mkoa wa DSM pale Msasani Club.Wakati wa kikao hicho viongozi wa muda walipewa majukumu mbalimbali kuhusina na klabu ambayo waliyafanya kwa ufanisi mkubwa sana na wa kipekee.Baadhi ya mafanikio ni pamoja na:

-Kuongeza idadi ya wanachama

-Kufanya vikao 4 vilivyo wakutanisha wana club wa mkoa wa dsm .
-Kufanya ziara ya kutembelea makumbusho ya kihistoria Bagamoyo.
-Kuwa karibu wana club wanaopata matatizo mbalimbali kama ugonjwa na hata sherehe. 
-Kujenga misingi imara ya club na kuhakikisha club inakuwa bora na yenye kufanikiwa katika kuelimisha,kufurahisha na kushirikiana.
Lakini wakati wa utekelezaji wa hayo yaliyotajwa hapo juu Uongozi ulikutana na changamoto mbalimbali ambazo zikifanyiwa kazi zitadumisha na kuifanya CLUB 19 kuwa group bora sana ambalo litajenga umoja na ushirikiano baina yetu.Uongozi wa muda kwa sasa unakuja na mapendekezo yafuatayo kwa ajili ya kuboresha club hii:
-Kusajili group hili litambulike kama organization rasmi serikalini.
-Kuwa na akaunti ya club ambayo.
-Kutafuta wafadhili wa club pale ambapo klabu inashiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii ikiwa na pamoja na klabu kushiriki matukio mbalimbali ya kijamii.
-Kujenga mahusiano na ma group mengine yenye mwelekeo mzuri kama wetu katika kushirikiana katika baadhi ya matukio hasa ya burudani.
- Kuchagua viongozi baada ya muda fulani maalum kupita ambao watakuwa tayari kuwatumikia watu.
Hivyo basi uongozi wa muda umeonelea kuwa ni vema sasa ukapatikana wa halisi wa kuchaguliwa wana club wote.Katika hili Uongozi wa muda unashauri yafanyike yafuatayo:
- kutaja tarehe ya kukutana na kuchagua viongozi
-kutoa maoni tuwe na uongozi wa aina ipi kwa maana ya mfumo upi na viongozi wawe madarakani kwa muda gani. 
-wenzetu wa mikoani kupendekeza majina ya watu wanaotaka wawe viongozi. 
-wadada washiriki katika kugombea nafasi za uongozi 
Kwa ujumbe huu sasa naomba yeyote atae comment hapa kuzingatia hayo yaliyoelekezwa maana uongozi wa muda utayapokea na kuweka maandishi.
Nawatakia kutoa maoni mazuri na kujenga karibuni

KNY-UONGOZI WA MUDA

No comments:

Post a Comment